MIEZI
michache baada ya mnyange wa Ilala 2009 ambaye alishiriki Miss Tanzania
mwaka huo, Sylvia Shally kujifungua, amenaswa laivu na njemba mmoja
ambaye jina halikupatikana akiwa ameshikana naye viuno kwa staili
zilizozua gumzo ikidhaniwa jamaa huyo ndiye baba mtoto wake, Amani
linafunguka. Tukio hilo lililoshuhudiwa na paparazi wetu, lilijiri
juzikati kwenye Mgahawa wa Nyumbani Lounge uliopo Kinondoni, Dar es
Salaam ambapo kulikuwa na ‘bethdei’ ya Miss Progress International
2010/11, Julieth William. Muda wote Sylvia alishuhudiwa akining’inia
kwenye mwili wa mshkaji huyo wakipapasana hapa na pale huku wakiendelea
kufanya shughuli ya ‘U-MC’ wa sherehe hiyo baada ya kukosekana kwa MC
na kusababisha minong’ono kwa wadau wakihoji kama jamaa ndiye baba mtoto
wake. Baada ya kujihakikishia utajiri wa picha za wawili hao,
paparazi wetu alimvuta Sylvia pembeni na kumuuliza na uhusiano gani na
mwanaume huyo au ndiye baba mtoto wake ambapo alifunguka: “Jamani kupiga picha na mtu ndiyo baba mtoto wako? Ni rafiki yangu tu wewe achana na hizo habari hazina maana yoyote.”
No comments:
Post a Comment