KAULI YA KWANZA YA DOGO JANJA BAADA YA KURUDISHWA KWAO NA MADEE.
Kama ulipitwa na hii stori ni
kwamba msanii Madee wa TipTop Connection ambae ndio alikabidhiwa kumlea
Dogo Janja na kumsimamia kwenye muziki alitangaza juzi kwamba
amemrudisha Dogo Janja kwenye mikono ya wazazi wake baada ya kuona
muelekeo wa Janja sio mzuri kitabia.
Alisema kwanza Janja alikua
mtoro wa shule na mara kadhaa hakwenda shule na alikua akimdanganya,
aliwahi kumkuta anaogoelea Ubungo Plaza wakati wenzake wako shule,
amekuta msg za matusi ambazo Dogo Janja aliwatumia watu wengine kuhusu
Madee na makosa mengine kadhaa.
Dogo Janja ambae sasa hivi
karudi Arusha tayari amefunguka kila kitu katika Interview ya Dakika 40
Exclusive on millardayo.com na yafuatayo hapo chini ni baadhi ya mambo
aliyoyazungumza.
Amesema “kwanza napenda
watanzania wajue kwamba mimi nilikua siishi na Madee nilikua naishi na
rafiki yake ambae ni Abdallah Doka Kimara jirani na Madee, Madee alikua
haniangalii kwa chochote na niliweka kikao juzi kati tu hapa nilikua
nataka nirudi kwetu, kula ni Doka, kuvaa Doka, Hela ya Shule Doka….
ninavyoongea hapa Dogo Janja sijawahi kulipwa hela zaidi ya laki tatu
kwenye show, Tanzania hii nimeshaizunguka ujue alafu sioni faida yake
nakwenda kwenye show nikirudi napewa laki moja alafu ukiuliza mtu
anaweza kukununia sasa nikawa zinanikera lakini nikawa nashindwa kuongea
sababu ndio niko pale kwa ajili ninasoma”
KUHUSU ACCOUNT YANGU BANK:
“Madee alininyang’anya mpaka kadi yangu ya ATM yani mimi narudi Arusha
ni kama nakwenda kuanza maisha mapya hamna ambacho useme labda narudi
Arusha ni kama vile nakwenda kuanza maisha mapya hamna ambacho useme
labda naweza kurudi Arusha labda kwenye account sijui nina shilingi
ngapi, kachukua hela zangu zote kwenye account yani, mi nilikua namuona
mwema ananijali aliniambia nenda kafungue account na kiuaminifu pale
unatakiwa kuandia namba zako mimi sikuandika zangu nikaandika za Madee,
taarifa yoyote ya bank inakutana na Madee, mi siwezi kumtusi yule
nitakua namkosea sana hata akinipa radhi inaweza kunipata mi naongea
kilicho moyoni mwangu mpaka nimechukua hatua hii”
KURUDISHWA KWANGU ADA SHULENI NA KIWANGO CHA PESA BANK:
“Na jina lote hili Dogo Janja nilikua narudishwa ada nyumbani,
nikachukua hatua nikaenda kufanya show ile hela yangu ya show baada ya
kurudi nakumbuka alitoa laki mbili na 60, hela ilikua yangu akaniambia…
Ahh Janja hapa sina hela nyingine nenda katoe kwenye account
nitakurudishia.. ni brother alafu mi namuheshimu sana, kadi yangu ya
bank yeye ndio alikua anaizuia lakini mwisho wa siku nakuja kuangalia
account yangu, mbona account haisomi? na kadi yangu yeye ndio alikua
nayo… Millard nakwambia ukweli wa mwenyenzi Mungu mimi account yangu
haikuwahi kufikisha shilingi milioni moja na kila show ninayofanya
nalipwa shilingi milioni moja, naongea mbele za mwenyenzi Mungu mimi
mtoto wa kiislamu naitwa Abdulaziz”
KUHUSU SHOW YA MWISHO KUIFANYA KABLA YA YEYE KUNIPIGA: Madee
alinipigia simu jumapili akiwa Iringa ambapo jumanne wenzangu walikua
wanaanza mtihani,nilimwambia niko na Hassan nyumbani kwa Tunda akasema
ana kaka yake Kibaha alikua na show ya CCM alikua anamtaka lakini akaona
hawezi na analove na bro akashindwa kukataa, roho ilikua inaniuma mimi
hapa mimi nakwenda kufanya show kwa laki moja… alafu hapo niko na backup
wangu nimempa elfu 20 mi nikabaki na elfu 80 alafu hiyo 80
anakupigia…. wee sikia elfu 50 hiyo kaweke bank, elfu 50 tumia…. mi
nikafanya kipeace tu nikaenda kwenye show huyo brother wake kachelewa
kuturudisha hapa saa saba usiku kwa sababu ujue mimi sina usafiri na
yule jamaa alikua anasubiri mishe zake zote zikamilike alafu asubuhi
nilikua natakiwa kuingia shule, kosa sio langu ni la huyo kaka yake
Madee.. sikwenda shule jumatatu sababu nilichelewa.. hivi hata wewe
Millard unaweza kulala saa saba ukaamka saa kumi??????! hiyo siku ndio
nilitakiwa kwenda kuchukua namba ya mtihani nikapangwe la dawati langu
ili jumanne nifanye mtihani, nilipoona nimechoka nilimpigia mwalimu wa
Darasa nikamwambia siwezi kwenda shule jumatatu akaniambia hamna neno mi
nikienda jumanne siku ya mtihani niende asubuhi nitapata”
JINSI MADEE ALIVYONIPIGA: Nilikua nyumbani kwa Tunda Man na Hassan ambae aliniacha baada ya kutumwa, nimekaa kidogo natoka hivi nakutana na Madee geitini hajaniuliza
chochote zaidi ya kuanza kunipig, kanichezeshea mikono kanipiga makofi
alafu kanidhalilisha yani mtaa mzima umekusanyana pale kwa Tunda Man, t
shirt ilichanika na akanikatalia kupanda kwenye gari… roho iliniuma
palepale alafu alivyonikatalia kupanda kwenye gari huku akiniambia
anikute nyumbani baada ya dakika tano, roho iliniuma nikasema haya yote
nayapata kwa sababu mimi ndio nataka na napenda muziki na napenda baadae
niwe na maisha bora, niliongea na wazazi wakaniambia nivumilie lakini
kiukweli nikasema siwezi tena kuishi Dar es salaam na leo June 13 2012
ndio siku ya mwisho kuishi Dar es salaam hapa ninavyoongea, jioni
niliitisha kikao nikampigia Doka, Madee, na kaka yangu huyu nikaulizwa
labda kuna kitu Madee hanifanyii mi nikashindwa kuongea nikasema bwana
mimi sitaki chochote mi nirudisheni kwetu ujue Millard mpaka mimi
nachukua maamuzi haya kwamba naomba nirudishwe kwetu, nimeomba nirudi
kiroho safi tu lakini nashangaa yeye anapokwenda kuongea mambo mengine
kwenye media, mi namshangaa yule ni mtu mzima anajielewa ujue, sasa mimi
sijui kwa nini amekua hivyo”
KUHUSU MADEE KUMUOMBA BABA YANGU ANIAMBIE NISIONGEE CHOCHOTE KWENYE MEDIA: “Alimpigia
simu baba ya kumuomba nisizungumze chochote kwenye media akidai kwamba
itakua aibu kwangu na kwake, mimi niko hewani lakini hakunipigia..
baadae nikapata simu kutoka kwa bro akaniambia niongee na mama
nilipoongea nae akaniambia Madee kasema nisiseme chochote kwenye radio,
sasa imefika jioni nikashangaa nikamsikia sasa nikajiuliza kwa nini
kaongea? na mimi siwezi kumpigia yule simu yani nimeshaapia kwa
mwenyeenzi Mungu siwezi kumpigia simu.
KUHUSU MIMI KUACHA MUZIKI:
“Roho inaniuma kichizi nimeona hiviii, yani huu mziki huu kwa sababu
haunisaidii chochote, mimi narudi Arusha ni kama narudi tena kuanza
maisha mapya kwa hiyo mimi nimeona bora tu kama inawezekana huu muziki
naweza kuacha na nitaishi kama zamani kwa sababu kwetu sijaua, nimeona
bora nitulie nyumbani ujue mpaka Millard pale nimeomba kabisa jamani
Eeehe nirudisheni nyumbani kwetu, nasema Inshallaah mwenyeenzi Mungu
yupo na mimi na riziki hapangi Madee riziki anapanga Mungu”
KUHUSU KUSOMA DAR ES SALAAM: “Sitaki kabisa kusoma Dar es salaam mimi nakwenda kusoma Arusha au mkoa wowote sitaki tena.
Hiyo ni sehemu tu alichokisema
Dogo Janja kuhusu yeye kuondoka kuwa chini ya Madee na kurudi nyumbani
kwao Arusha, mengine utaendelea kuyasikia kupitia AMPLIFAYA ya CLOUDS FM
leo saa moja usiku na pia hapa millardayo.com! kuna picha za hizo msg
pamoja na msg ya mwisho Janja kumtumia Tunda Man, vyote ni Exclusive on
millardayo.com
No comments:
Post a Comment